1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiEthiopia

Ethiopia kuanza awamu ya nne ya kujaza bwawa lenye utata

22 Juni 2023

Ethiopia inajiandaa kuzindua awamu ya nne ya ujazaji maji katika bwawa lake kubwa kwenye Mto Nile, licha ya upinzani kutoka kwa jirani yake Misri.

Äthiopien Mega-Damm -  Grand Ethiopian Renaissance Dam  GERD
Picha: Minasse Wondimu Hailu/AA/picture alliance

Naibu Waziri Mkuu wa Ethiopia Demeke Mekonnen ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje, amesema kuwa mradi huo wa bwawa kubwa lenye thamani ya Dola bilioni 4.2, uko mbioni kukamilika baada ya kujazwa maji kwa awamu tatu za mwanzo.

Soma pia: Ethiopia yaanza tena kujaza bwawa la Grand Renaissence

Bwawa hilo limekuwa chanzo cha migogoro ya kikanda tangu Ethiopia ilipozindua mradi wake mwaka 2011. Misri na Sudan mara kwa mara zimeitaka Ethiopia kusimamisha zoezi la kujaza maji bwawa hilo, zikitaja kuwa ni kitisho kwasababu ya kutegemea maji ya Mto Nile.

Ethiopia kwa upande wake inadai kwamba endapo mradi huo utakamilika utaweza kuchangia pakubwa katika uzalishaji wa umeme na maendeleo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW