1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEthiopia

Ethiopia na waasi wa TPLF kuunda chombo cha kusimamia amani

23 Desemba 2022

Serikali ya Ethiopia na vikosi vya waasi wa Tigray wamekubaliana kuanzisha chombo cha pamoja cha kufuatilia na kuhakikisha mpango wa amani wa kumaliza vita unaheshimiwa na pande zote.

 Released Ethiopian National Defence Force ENDF Prisoners of War from Mekele center
Picha: DW

Mwezi Novemba pande hizo hasimu zilitangaza kusitisha mapigano kwenye jimbo la kaskazini la Tigray, ambako maelfu ya watu wameuawa katika mapigano ya miaka miwili.

Miongoni mwa masharti ya makubaliano hayo ni kipengele cha kuanzisha chombo cha kufuatilia na kuzingatia ili pande zote mbili ziwe na uhakika kwamba mpango huo unafanikishwa.

Hilo lilikamilishwa jana na makamanda wa jeshi kutoka serikali ya Ethiopia na kundi la Wapiganaji wa Ukombozi wa Watu wa Tigray, TPLF, katika mkutano uliofanyika kwenye mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Pembe ya Afrika, IGAD, Workneh Gebeyehu, amesema kuanzishwa kwa chombo cha pamoja ni  "ushuhuda wa wazi" wa pande zote kuheshimu makubaliano ya amani.