Hatimaye shirika la ndege la Ethiopia limeanzisha tena safari zake nchini Eritrea. Ni hatua nyingine ya kurejesha mahusiano baina ya mataifa hayo yaliyohasimiana kwa muda mrefu. Ilikuwa shamrashamra na furaha kubwa kwa abiria waliosafiri safari hii ya kwanza kutoka Ethiopia kwenda Eritrea. Vidio hii ina matukio yote.