Ethiopia yadai vikosi Tigray vyajiandaa kwa mashambulizi
12 Juni 2026
Matangazo
Katika mahojiano na shirika la habari la AFP naibu kiongozi wa Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray TPLF Amanuel Assefa, amesema madai hayo ni "si ya kweli kabisa.
Assefa alidai kuwa serikali inajiandaa kuanzisha vita dhidi ya Tigray na inataka kutumia kisingizio hicho kuupotosha jumuiya ya kimataifa.
Hapo jana , serikali ya nchi hiyo ilidai kuwa vikosi vya Tigray vilikuwa vinajiandaa kuanzisha mashambulizi dhidi yake katika siku zijazo, jambo lililoibua hofu ya kurejea kwa vita.
Pia iliishtumu TPLF kwa kuimarisha uhusiano wake na Eritrea, ingawa kundi hilo limekanusha madai hayo.