Ethiopia yaituhumu Eritrea kwa kujiandaa kwa vita
8 Oktoba 2025
Haya ni kwa mujibu wa barua kutoka kwa wizara ya mambo ya kigeni ya nchi hiyo iliyoonekana na Shirika la Habari la Ufaransa AFP.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ethiopia amemwandikia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, akimueleza kuwa ushirikiano kati ya serikali ya Eritrea na chama cha TPLF ambacho kimepigwa marufuku ya kushiriki siasa kwa miaka 30, umekuwa wazi katika miezi michache iliyopita na kwamba wanapanga kuanzisha vita dhidi ya Ethiopia.
Ethiopia vile vile inaituhumu Eritrea na TPLF kwa kufadhili, kuhamasisha na kuyaelekeza makundi yenye silaha katika eneo la Amhara, ambako jeshi la Ethiopia limekuwa likikabiliana na waasi kwa miaka kadhaa. Kwa miezi kadhaa sasa, mahusiano kati ya majirani hao wawili Ethiopia na Eritrea yamevurugika.