SiasaEthiopia
Ethiopia yakamilisha ujenzi wa bwana la umeme Mto Nile
4 Julai 2025
Matangazo
Tangazo hilo la Abbiy ni hatua kubwa ya utawala wake iliyoiingiza Addis Ababa kwenye mzozo mkubwa na Misri juu ya ugawanaji sawa wa maji kati yao.
Akiwahutubia wabunge hapo jana, Abbiy alisema serikali sasa inaandaa uzinduzi rasmi wa mradi huo mkubwa wa umeme barani Afrika katika mwezi Septemba.
Waziri mkuu huyo alisema atahakikisha kuwa maendeleo ya nchi yake hayaziathiri nchi jirani za Misri na Sudan, kwani maendeleo ya mmoja yanapaswa kuwa ya wote.
Kwa miaka kadhaa, Cairo na Addis Ababa zimekuwa zikilumbana juu ya ujenzi wa bwawa hilo lenye thamani ya dola bilioni nne ulioanza mwaka 2011.