1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEthiopia

Ethiopia yamteua afisa wa TPLF kuongoza Tigray

23 Machi 2023

Serikali ya Ethiopia imemteua afisa wa ngazi ya juu wa chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray, TPLF kuwa mkuu wa serikali ya mpito ya Tigray, baada ya mpango wa amani kuvimaliza vita vilivyodumu kwa miaka miwili.

Äthiopien, Tigray Konflikt, Getachew Reda von TPLF
Picha: Yasuyoshi Chiba/AFP

Waziri Mkuu Abiy Ahmed, amemteua Getachew Reda, kuwa rais wa utawala wa jimbo la Tigray. Tangazo hilo limetolewa leo siku chache baada ya bunge kukiondoa chama cha TPLF katika orodha ya makundi ya kigaidi.

Getachew, mshauri wa kiongozi wa TPLF, Debretsion Gebremichael, aliwahi pia kuwa Waziri wa Mawasiliano wa serikali ya shirikisho la Ethiopia chini ya utawala wa Waziri Mkuu, Hailemariam Desalegn aliyetawala kuanzia mwaka 2012 hadi 2018.