1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ethiopia yamtuhumu Trump kwa kuchochea vita

24 Oktoba 2020

Ethiopia imemtuhumu rais wa Marekani Donald Trump kwa kuchochea vita kuhusu bwawa la moto Nile baada ya rais huyo kuzungumza dhidi ya mradi huo na kusema Misri inaweza kuuharibu. Ethiopia imemtuhu pia Trump kwa upendeleo

Äthiopien Fernsehansprache Abiy Ahmed, Ministerpräsident
Picha: Ethiopian Broadcasting corporation

Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Gedu Andargachew alimuita balozi wa Marekani Michael Raynor kutoa ufafanuzi juu ya matamshi ya Trump, yanayoashiria hatua ya karibuni ya kujiingiza kwa rais huyo katika mzozo nyeti wa muda mrefu kati ya Ethiopia na mataifa jirani ya Sudan na Misri.

Gedu alimuambia Raynor kwamba "uchochezi wa vita kati ya Ethiopia na Misri na rais alieko madarakni nchini Marekani hauakisi ushirikiano wa muda mrefu na ushirika wa kimkakati kati ya Ethiopia na Marekani, na wala haukubaliki katika sheria ya kimataifa inayoongoza uhusiano baina ya mataifa," ilisema wizara ya mambo ya nje katika taarifa.

Soma pia: Misri, Sudan zasitisha mazungumzo na Ethiopia

Ethiopia ilikuwa inajibu matamshi kuhusu bwawa, maarufu kama Grand Renaissance, yaliotolewa na Trump siku ya Ijumaa, wakati wa hafla ya kuadhimisha mafanikio ya kusawazisha uhusiano kati ya Israel na Sudan.

Bwawa la Grand Renaissance linalozua mtafaruku kati ya Ethiopia, Misri na Sudan.Picha: DW/Negassa Desalegen

Matamshi hayo yalitolewa saa chache baada ya Trump kufanya mazungumzo kwa njia ya simu na waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok, na walitoa wito wa suluhu la kirafiki kati ya Ethiopia na Misri.

'Misri italipua bwawa'

Katika simu hiyo iliyopigwa mbele ya waandishi habari katika ikulu ya White House, Trump alisema ameipa Misri ushauri huo huo, na kuongeza kuwa hali imekuwa ya hatari. Aidha Trump ameonya kwamba Misri inaweza kuishia kulilipua bwawa hilo.

"Ni hali ya hatari sana kwa sababu Misri haitoweza kuishi namna hiyo," Trump aliwambia waandishi habari katika ofisi yake ya White House.

Wataishia kwa kulipua bwawa hilo. Na nilisema na nalisema wazi -- watalipua bwawa hilo. Na laazima wafanye jambo," Trump alisema.

Soma pia: Ethiopia, Misri, Sudan zakubali kuahirishwa ujazaji wa bwawa la Nile

Ofisi ya waziri mkuu Abiy ilitoa taarifa Jumamosi  ikiteeta bwawa hilo na kubainisha kwamba Ethiopia ilikuwa imejifunga kwa mazungumzo yanayoongozwa na Umoja wa Afrika, ambayo ilisema "yamepiga hatua muhimu."

Ris Donald Trump alipotangaza kuiondoa Sudan kwenye orodha ya mataifa yanayofadhili ugaidi, na pia kusema kuitaka Ethiopia ikubaliane na Misri kuhusu bwawa lake.Picha: Alex Edelman/AFP/Getty Images

"Pamoja na hayo, matamshi ya nyakati fulani ya kutoa vitisho ili kuifanya Ethiopia isalimu amri kwa masharti yasiyo ya haki yanaendelea kutolewa. Vitisho hivi dhidi ya mamlaka ya Ethiopia vimeshauriwa vibaya, havina manufaa na ni ukiukaji wa wazi wa sehria ya kimataifa," ilsiema taarifa hiyo.

Nakala tofuati ya tamko iliyotolewa kwa lugha ya Amharic, ilikuwa na maneno makali zaidi.

"Kuna ukweli wa aina mbili ambao dunia imeuthibitisha. Kwamba hakuja kuwa na mtu alieishi kwa amani baada ya kuichokoza Ethiopia. Wa pili ni kwamba ikiwa Ethiopia inasima pamoja kwa lengo moja,  hakuna shaka kwamba itaibuka mshindi," lilisema.

Soma pia: Maafisa wa Misri, Ethiopia na Sudan kukutana Marekani?

Juhudi za Washington kuongoza makubaliano kutatua suala la bwawa ziliishia kwa kushindwa mwaka huu baada ya Ethiopia kuutuhumu utawala wa  Trump kwa kuipendelea Misri.

Marekani ilitangaza  mwezi uliyopita kwamba insitisha sehemu ya msaada wake wa kifedha kwa Ethiopia, ikielezea kukosena kwa maendeleo katika mazungumzo na uamuzi wa upande mmoja wa Ethiopia, kuanza kujaza hifadhi ya maji ya bwawa hilo.

Upendeleo kwa Misri

Maafisa wengi wa Ethiopia wanamuona Trump kama mtu aliezibwa macho na ushirika wake na rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi.

"Samahani kusema haya lakini bwana huyi hajui kabisaa anachozungumzia. Ethiopia na wa Ethiopia kamwe hawatatishiwa na matamshi ya kizembe kama hayo," alisema mtangulizi wa Abiy Hailemriam desalegn, katika ujumbe wa Twitter.

Mkuu wa sera ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell, alisema katika taarifa siku ya Jumamosi kwamba makubaliano kuhusu bwawa hilo yalikuwa yanakaribiwa kufikiwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW