1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiEthiopia

Ethiopia yapinga ripoti ya HRW kuhusu safisha ya Watigray

6 Juni 2023

Serikali ya Ethiopia imepinga ripoti ya Shirika la Human Rights Watch inayowatuhumu maafisa wa serikali na vikosi vya kikanda kwa kuendesha kile lilichokiita kampeni ya "safishasafisha ya kikabila".

Residents in Tigray region demonstrate to go back to their home
Picha: Million Hailesilassie/DW

Serikali ya Ethiopia imepinga ripoti ya Shirika la Kutetea Haki za Binaadamu la Human Rights Watch inayowatuhumu maafisa wa serikali na vikosi vya kikanda kwa kuendesha kile lilichokiita kampeni ya "safishasafisha ya kikabila" magharibi mwa Tigray licha ya makubaliano ya amani ya mwaka jana. Taarifa ya Idara ya Mawasiliano ya Serikali ya Ethiopia - GCS imesema tuhuma hizo hazijaambatanishwa na ushahidi. Imeongeza kuwa ripoti hiyo ya kupotosha hali halisi inajaribu kuhujumu msingi wa watu kuishi pamoja kwa amani na kuchochea mzozo wa kikabila na kuzuia juhudi za kitaifa za amani na maridhiano. HRW ilisema katika ripoti yake ya Juni mosi kuwa makubaliano ya amani yaliyofikiwa Novemba kuumaliza mzozo uluiodumu kwa miaka miwili katika mkoa wa Tigray hayajasitisha safishasafisha ya kikabila katika eneo linalogombaniwa la magharibi mwa mkoa huo. Lilisema vikosi vya usalama vya Amhara na maafisa wa mpito wanaendesha kampeni inayowalenga wakaazi wa Tigray, kwa kufanya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinaadamu.