1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ETHIOPIA YATAWAZWA MABINGWA WAPYA WA CHALLENGE CUP

Ramadhan Ali27 Desemba 2004

PREMIER LEAGUE (LIGI YA UINGEREZA) ILIKUA UWANJANI NA CHELSEA IMESHIKA USUKANI

ETHIOPIA NI MABINGWA WAPYA WA CHALLENGE CUP- KOMBE LA AFRIKA MASHARIKI NA KATI (ETHIOPIA 3 BURUNDI 0)

NA MABINGWA WA UJERUMANI WEDER BREMEN WAMRANDIA SASA SHABANI NONDA NAHODHA WA CONGO

Ligi ya Ujerumani-Bundesliga ikiwa likizoni kwa siku kuu za x-masi na mwaka mpya hadi januari 22, klabu bingwa Werder Bremen, hatahivyo, imegonga vichwa vya habari mwishoni mwa wiki:

Bremen imemuuza mshambulizi wake –mgiriki Angelos Charisteas kwa Ajax Amsterdam ya Uholanzi.

Chipukizi huyo wa miaka 24 utakumbuka ndie alietia lile bao la ushindi lililoitawaza kati ya mwaka huu Ugiriki mabingwa wa Ulaya mbele ya Ureno.Ameuzwa kwa kitita cha Euro milioni 4.9 kwa kipindi cha miaka 4.Ajax Amsterdam baadae ilithibitisha mpango huo.

Mabingwa wa ujerumani Wrdre Bremen sasa wanamrandia mshambulizi na nahodha wa Kongo Shabani Nonda licha ya kuwa ameumia wakati huu kujaza pengo aliloliacha Charisteas.Shabani Nonda anaichezea wakati huu Monaco,nchini Ufaransa.

Katika Ligi ya Uingereza,ambayo kinyume na Ligi kadhaa haiendi likizoni kwa siku kuu za X-masi na mwaka mpya, Chelsea na mahasimu wao Arsenal zilitamba.Chelsea ilishinda nyumbani dhidi ya Aston Villa wakati Arsenal ilinguruma mbele ya Fulham jana.Thierry henry alitia bao lake la 20 kwa Arsenal na Robert Pires akaaongezea la pili kuipa ushindi Arsenal.Chelsea inayoongoza orodha ya Ligi kwa jumla ya pointi 46 kwa 41 za Arsenal iliilaza Aston Villa. manchester United iko nafasi ya 4 ya ngazi ya Ligi ya Uingereza.

ETHIOPIA NDIO MABINGWA WAPYA WA KOMBE LA AFRIKA MASHARIKI NA KATI:

Wakicheza nyumbani jumamosi, Ethiopia waliizaba Burundi mabao 3:0 na kulibakisha Kombe nyumbani.Mabao ya Nigussie mnamo dakika ya 21 ya mchezo, Tesfaye dakika ya 31 na Alemerew dakika ya 48 yalitosha kuikomoa Burundi na kuirejesha Bujumbura mikono mitupu.

Kwa ushindi huo wa Ethiopia, Kombe la 28 la Challenge Cup limemalizika.Hatahivyo, pongezi nyingi kwa kocha wa Burundi Maulidi Ramadhan alieijenga upya timu ya Burundi akiegemea wachezaji chipukizi kufuatia msukosuko wa uongozi nchini.Katika kikosi chake alikuwamo Saidi Ntibazonkizia,mwenye umri wa miaka 15 na mchezaji mchanga kabisa katika mashindano hayo.

Kipindi cha kwanza Ethiopia ikiongoza tayari kwa mabao 2:0 mbele ya mashabiki wa nyumbani 40.000.

Kuibuka m akamo-bingwa wa Challenge Cup kumepokewa vipi nyumbani Bujumbura ?

Kombe la Challenge Cup kwa mataifa likiwa limemalizika kwa ushindi wa Ethiopia, lile la klabu bingwa kwa Afrika mashariki na kati litaanza nchini Tanzania kati ya Februari 13 na 28 mjini Arusha na Mwanza.

Mabingwa wa Kenya Ulinzi Stars,wameruhusiwa mwishoe kuiwakilisha Kenya licha ya kufungiwa kwao kwa miaka 3 kucheza katika dimba barani Afrika.CAF-shirikisho la dimba la Asfrika limeifungia Ulinzi Stars kwa kutotimiza miadi yake kucheza na VITA CLUB ya Kongo katika changamoto za Kombe la klabu bingwa mjini Kinshasa, mapema mwaka huu.

Mabingwa wa sasa wa Kombe hili ni APR ya Rwanda.Timu nyengine zitakazoania Kombe hilo ni Simba Sports Club ya Tanzania-bara,KMKM ya Zanzibar,Villa ya Uganda,El Hilal ya Sudan,Adulis ya Eritrea,Gendermarie ya Djibouti,Awasa ya Ethiopia,Rayon Sport ya rwanda na Muzinga ya Burundi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW