1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ethiopia yawahamisha maelfu kutokana na kitisho cha volkano

Sylvia Mwehozi
4 Januari 2025

Maelfu ya raia katika eneo la ndani la kaskazini mashariki mwa Ethiopia wamelazimika kuhamishwa kutokana na kitisho cha kutokea mlipuko wa volkano.

Muonekano wa juu wa eneo hai la volcano ya Erta Ale mkoani Afar
Muonekano wa juu wa eneo hai la volcano ya Erta Ale mkoani AfarPicha: Roberto Moiola/robertharding/picture alliance

Maelfu ya raia katika eneo la ndani la kaskazini mashariki mwa Ethiopia wamelazimika kuhamishwa kutokana na kitisho cha kutokea mlipuko wa volkano.

Zoezi hilo linafanyika baada ya mitikisiko kadhaa midogo kushuhudiwa tangu siku ya Alhamisi kutoka katika Mlima Dofen na kuzua hofu ya mlipuko kamili wa volkano ambayo inaweza kuweka watu wengi hatarini.

Soma: Mapigano mapya yaripotiwa katika jimbo la Afar, Ethiopia

Kulingana na idara ya usimamizi wa maafa katika mkoa wa Afar, tope la volkano linalotiririka kutoka mlima Dofen limesababisha nyufa kubwa kwenye miundombinu muhimu, ikiwemo barabara kuu na kuharibu mali.

Afar ni mojawapo ya maeneo kame na yenye joto zaidi nchini Ethiopia, yenye historia ya milipuko ya volkano na matetemeko ya ardhi ya mara kwa mara.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW