1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ethiopia yawauwa watu 42 waliofanya mauaji ya watu 100

24 Desemba 2020

Wanajeshi wa Ethiopia wamewauwa watu 42 wenye silaha wanaoshukiwa kufanya mauaji ya watu 100 kwenye jimbo la magharibi la Benishangul-Gumuz.

Äthiopien Alamata Amhara Special Forces
Picha: Eduardo Soteras/AFP/Getty Images

Kituo cha kimoja cha televisheni chenye mafungamano na serikali ya Ethiopia, kimeripoti kuwa wanajeshi wa nchi hiyo pia wamekamata silaha za jadi ikiwemo rungu na mishale iliyokuwa ikitumiwa na wapiganaji hao kuendesha mashambulizi.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Picha: Amanuel Sileshi/AFP

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abey Ahmed alisema mapema leo kuwa anawatuma wanajeshi zaidi kwenye mkoa huo unaopakana na Sudan kwa lengo la kuchukua jukumu la ulinzi siku moja tangu watu wenye silaha wasiojulikana kuwauwa watu 100 kwenye kijiji kimoja jimboni humo

"Mauaji ya raia jimboni Benishangul-Gumuz ni janga baya" aliandika Abiy kwenye ukurasa wake wa Twitter na kuongeza " kwa serikali kutatua mzizi wa sababu za janga hilo, imetuma idadi inayohitajika ya jeshi"

Ethiopia imekuwa ikiandamwa na machafuko ya kila wakati tangu Abiy alipochukua madaraka mwaka 2019 na kuongeza kasi ya mageuzi ya kidemokrasia ambayo yamepunguza nguvu ya udhibiti wa dola kwa pande hasimu za kisiasa nchini humo

Jimbo la Benishangul-Gumuz aghalabu hukumbwa na machafuko 

Picha: Burayu City Administration Office

Kituo cha televisheni cha FANA kimesema jeshi limewauwa watu 42 wenye ishara ya "kupinga amani", bila hata hivvyo kufafanua ni lini makabiliano hayo yalitokea au kuwataja watu waliouwawa.

Ikiwanukuu maafisa wa kieneno, kituo hicho kimeashiria watu wenye silaha walihusika na shambulizi la siku ya Jumatano kwenye kaunti ya Bulen.

Hapo jana Jumatano, tume ya haki za binadamu inayosimamiwa na serikali ilisema zaidi ya watu 100 waliuawa katika kijiji cha Bekoji kaunti ya Bulen ambako wakaazi wake wengi ni mchanganyiko wa jamii mbalimbali.

Watu kadhaa walioshuhudia mauaji hayo wamesema nyumba pia zilichomwa moto na kwamba watu wengine walidungwa na silaha zenye ncha kali.

Shirika la habari linalomilikiwa na serikali nchini humo, limeripoti kuwa maafisa 5 wakuu katika jimbo hilo pia wametiwa nguvuni kuhusiana na masuala ya usalama wa eneo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW