Eto’o amtetea hadharani Infantino
24 Agosti 2026
Matangazo
Eto'o, ambaye ni rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon, amesema haoni kosa lolote alilofanya Infantino, akidai upinzani dhidi yake umechochewa zaidi na siasa kuelekea uchaguzi wa urais wa FIFA mwakani.
Aidha amesema Infantino amebadilisha soka kwa kutoa nafasi kwa mataifa madogo kushiriki Kombe la Dunia na kusaidia mashirikisho ya Afrika kuendelea kwa kasi. Mashirikisho ya Afrika kupitia CAF tayari yamemuunga mkono Infantino.
Infantino anakabiliwa na uwezekano wa kura ya kutokuwa na imani, huku mijadala kuhusu mustakabali wa FIFA ikiendelea kupamba moto.