1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU ina wasiwasi na hatma ya mapigano Nagorno Karabakh

12 Oktoba 2020

Umoja wa Ulaya umeelezea wasiwasi wake kuhusiana na ripoti za ukiukaji makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya mataifa jirani yaliyo hasimu ya Armenia na Azerbaijan yanayowania udhibiti wa jimbo la Nagorno Karabakh

Bosnien Herzegowina | Milorad Dodik, Šefik Džaferović und Željko Komšić
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borell Picha: Marina Maksimović/DW

Taarifa iliyotolewa na mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Jossep Borell, imesema kanda hiyo inatiwa shaka na operesheni za kijeshi zinazoendelea ikiwemo zinazohujumu maeneo ya makaazi na kuwalenga raia.

Taarifa hiyo Borell imetolewa baada ya kuvunjika kwa sehemu fulani makubaliano ya kusitisha mapigano baada ya kuzuka upya kwa makabiliano huku kila upande ukiulaumu mwingine kuhusiana na kilichotokea.

Borell amesema Umoja wa Ulaya unatoa wito kwa Armenia na Azerbaijan kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano na kuanza mazungumzo chini ya upatanishi wa kundi  liitwalo OSCE Minsk linaloongoza juhudi za kumaliza mzozo wa Karabakh.

Pande hizo mbili zilifikia makubaliano ya kusitisha mapigano, kubadilishana wafungwa na miili ya wale waliouwawa katika mapambano ya wiki mbili kuwania udhibiti wa jimbo la Nagorno Karbakh.

Mji wa Ganja washambuliwa 

Majengo yaliyoharibiwa katiia mji wa Ganja, Azerbaijan Picha: Umit Bektas/Reuters

Hata hivyo jana wizara ya mambo ya kigeni ya Azerbaijan ilisema vikosi vya Armenia vilifanya mashambulzi makali ya usiku kucha kwenye mji wa pili kwa ukubwa wa Ganja, yaliyowauwa watu 7 na kujeruhiwa wengine 33.

Mmoja ya walio shuhudia kisa hicho amesema waliamshwa na sauti kubwa ya mlipuko uliosambaratisha upande mmoja wa jengo la ghorofa mbili na kuharibu nyumba 9.

"Tuliamini katika usitishaji mapigano. Tuliamini kuwa hiki hakitatokea, ndiyo maanda tulirejea nyumbani. Wasingerejea kama kusingekuwa na usitishaji mapigano. Waliokuwa wakiogopa. Nani angetaka vurumai hii? Kaka yangu ana nyumba mbili lakini hawana hata moja ya kuweza kuishi hivi sasa. Tunashukuru serikali na msaada wanaotupatia. Mungu atamsaidia kila mmoja". amesema.

Tukio la kushambuliwa kwa mji wa Ganja limetokea chini ya saa 24 tangu kuanza utekelezaji wamakubaliano ya kusitisha mapigano na kwa jumla limeyaweka  rehani makubaliano yenyewe.

Lawama za kila upande zaweka rehani usitishaji mapigano 

Picha: Sputnik/dpa/picture alliance

Madai ya ukiukaji makubaliano tayari yamesababaisha Armenia na Azerbaijan kusitisha mpango wa kubadilishana miili ya watu waliouwawa kwenye makabiliano ya siku zilizopita.

Msemaji wa vikosi vya Armenia aliandika kupitia ukurasa wa Facebook kuwa Azerbaijan imeshambulia makaazi ya watu kwenye jimbo la Karabakh .

Katika hatua nyingine maelfu ya watu waliandamana mjini los Angeles Marekani jana kulaani dhima ya Azerbaijan na Uturuki na kile waandamanaji wamekiita uchokozi wa nchi hizo mbili dhidi ya Armenia katita mzozo wa Karabakh.

Makundi ya watu yalikusanyika mbele ya ubalozi mdogo wa Uturuki mjini Los Angeles wakipeperusha bendera za Armenia huku wakipaza sauti za kuiunga mkono Armen.

Hayo yanajiri wakati duru kutoka mjini Brussels zimearifu kuwa mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Umoja wa Ulaya watakwua na mkutano leo kutafuta msimamo wa pamoja kuhusu masuala kadhaa ya kigeni ikiwemo mzozo kati ya Armenia na Azerbaijan.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW