1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya wakaribia kuidhinisha mkopo kwa Ukraine

22 Aprili 2026

Umoja wa Ulaya umetoa idhinisho la awali la mkopo wa euro bilioni 90 kwa Ukraine, baada ya mvutano wa miezi kadhaa kati ya Ukraine na Hungary kuhusu bomba la mafuta la Druzhba lililoharibiwa.

Makao Makuu ya Umoja wa Ulaya, Brussels
Umoja wa Ulaya uko katika hatua za awali za kuipa Ukraine mkopo wa euro bilioni 90Picha: Stephanie Lecocq/REUTERS

Hungary iliuzuia uamuzi huo hadi Ukraine itengeneze bomba hilo. Baada ya Ukraine kukiri matengenezo yamekamilika Hungary ilipewa saa 24 kutoa idhini ya mwisho.

Kuondoka kwa Orban madarakani chanzo cha ahueni kwa Ukraine

Mgogoro huo ulisababisha mvutano kati ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, na kuchelewesha fedha ambazo Ukraine inazihitaji sana kufidia nakisi ya bajeti wakati vita na Urusi vinaendelea.

Endapo idhini ya mwisho ya mkopo huo itatolewa, Umoja wa Ulaya utaanza kutoa fedha hizo katika miezi ijayo. Mgogoro huo pia ulikuwa umezuia vikwazo vipya vya EU dhidi ya Urusi, ambavyo sasa vinaweza kuidhinishwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW