1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU kuipatia Ukraine bilioni 90 kwa miaka miwili

3 Desemba 2025

Mkopo wa Euro bilioni 90 kwa miaka miwili unalenga kuipatia Ulaya sauti yenye nguvu katika mazungumzo ya kutafuta amani ya Ukraine

Rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen na mkuu wa shirika la nishati la Kimataifa Fatih Birol
Rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen na mkuu wa shirika la nishati la Kimataifa Fatih BirolPicha: Harry Nakos/AP Photo/picture alliance

Rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, amewasilisha mpango wa kuipatia Ukraine  Euro bilioni 90 kwa kipindi cha miaka miwili.

Mpango huo unadhamiriwa kuuwezeshaUmoja huo wa Ulaya  kuwa na sauti yenye nguvu katika kuongoza majadiliano ya kutafuta amani Ukraine.

Mkopo huo kwa Ukraine kwa mujibu wa mpango uliowasilishwa, utafadhiliwa kutoka Umoja wa Ulaya au kwa fedha zitakazotokana na mali za Urusi zinazoshikiliwa katika nchi za Umoja huo. Pendekezo la kutumiwa mali za Urusi limepingwa vikali na Ubelgiji.

EU inavyopanga kutumia mali za Urusi kusaidia Ukraine

Wakati huohuo Ukraine na Urusi zimesema ziko tayari kwa mazungumzo zaidi na Marekani kuhusu kumaliza vita, baada ya kukosa kupatikana mwafaka kwenye mazungumzo yaliyofanyika jana kati ya mjumbe maalum wa Marekani, Steve Witkoff, Jared Kushner na rais Vladmir Putin.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW