EU: Makampuni yatakayosababisha athari za kijamii kuwajibika
14 Desemba 2023Haya yametangazwa leo katika chapisho la kamati hiyo kupitia mtandao wa kijamii wa X.
Chini ya makubaliano hayo yalioafikiwa leo asubuhi mjini Strasbourg, Ufaransa, makampuni ya ukubwa fulani katika Umoja wa Ulaya, yatahitajika kufuatilia na kushughulikia masuala kamaajira kwa watoto, utumwa, unyanyasaji wa wafanyakazi, uchafuzi wa mazingira, uharibifu wa mazingira na viumbe hai katika hatua mbalimbali za mchakato wa uzalishaji bidhaa zao katika nchi mbali mbali.
Soma pia:Umoja wa Ulaya wakubaliana juu ya sheria muhimu ya AI
Sheria hizo mpya pia zitatumika kwa mashirika ya kimataifa yanayofanya biashara muhimu katika Umoja wa Ulaya.
Mara baada ya kupitishwa, Ujerumani inatarajiwa kuimarisha sheria zake zilizopo.
Makubaliano hayo bado yanapaswa kuthibitishwa na bunge la Ulayana matifa wanachama lakini huu ni utaratibu wa kawaida.