1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU na nchi za Ghuba watoa wito wa mazungumzo kusitisha vita

5 Machi 2026

Umoja wa Ulaya na Baraza la Ushirikiano la Mataifa ya Ghuba, GCC, Alhamis wametoa wito wa mazungumzo na diplomasia kwa ajili ya kuutatua mzozo wa Mashariki ya Kati.

Mwakilishi wa masuala ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas akizungumza Brussels
Mwakilishi wa masuala ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas akizungumza BrusselsPicha: Dursun Aydemir/Anadolu/picture alliance

Katika taarifa ya pamoja Umoja wa Ulaya na GCC wamesema kuwa nchi za Ghuba zina haki ya kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Iran.

Haya yanakuja wakati ambapo Italia imekuwa taifa la hivi karibuni kutoka Ulaya baada ya Uhispania kuvikosoa vita vya Iran vilivyosababishwa na mashambulizi ya Marekani na Israel.

Waziri wa ulinzi wa Italia Guido Crosetto amesema mashambulizi hayo yamekiuka sheria ya kimataifa. Crosetto ameyasema hayo licha ya kuwa serikali ya mrengo wa kulia ya Italia inatafuta kuwa na mahusiano ya karibu na Rais wa Marekani Donald Trump.

Hayo yakijiri Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema mwito wa Israel wa kuwataka raia wa kusini mwa Lebanon kuyahama makaazi yao, "ni ukiukaji mkubwa wa sheria za vita."

Human Rights Watch limeyasema haya baada ya Israel kudai kwamba itafanya operesheni ya kijeshi katika maeneo hayo.

Lebanon imeburuzwa katika vita hivyo vya Mashariki ya Kati baada ya wanamgambo wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran kuanza kuishambulia Israel.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW