1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU wafikia makubaliano ya kuipatia fedha zaidi Ukraine

Sylvia Mwehozi
1 Februari 2024

Viongozi wa mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya hatimaye wameafikiana leo kuipatia Ukraine msaada mpya wa Euro bilioni 50 katika kusaidia uchumi wake ulioharibiwa na vita, licha ya kitosho cha Hungary kupinga mpango huo.

Brussel Ubelgiji | Viongozi wa Umoja wa Ulaya
Viongo wa Umoja wa Ulaya wakiongozwa na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen.Picha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel, ametangaza kwamba makubaliano hayo yamefikiwa ndani ya saa moja baada ya kuwasilishwa mjini Brussels.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyamekaribisha makubaliano hayo aliyoyataja kuwa ni uamuzi muhimu. 

Soma pia:Viongozi wa Umoja wa Ulaya wakabiliana na Orban kuhusu msaada wa Ukraine

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban, aliandika kupitia ukurasa wa X kwamba watasimama kwa ajili ya sauti ya watu hata kama wanapokea vitisho kutoka ndani ya Umoja huo.

Orban alizusha pingamizidhidi ya mpango wa kuisadia kifedha Ukraine mnamo mwezi Desemba na kutishia kuzuia kupitishwa kwake. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW