1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Eu wajadili kuipatia mkopo mpya Ukraine

23 Februari 2026

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa EU wanajadili hatua ya kuipatia mkopo mpya Ukraine wakati hungary ikitishia kutumia Veto kupinga hatua hiyo na vikwazo kwa Urusi

Mkuu wa sera za kigeni wa EU  Kaja Kallas kabla ya mkutano wa Brussels kuhusu kuipatia mkopo mpya Ukraine
Mkuu wa sera za kigeni wa EU Kaja Kallas kabla ya mkutano wa Brussels kuhusu kuipatia mkopo mpya UkrainePicha: Virginia Mayo/AP Photo/picture alliance

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanakutana hivi leo mjini Brussels, kujadili mpango wa kuipatia mkopo mwingine Ukraine pamoja na awamu  nyingine ya vikwazo dhidi ya Urusi.

Mazungumzo hayo yanafanyika siku moja kabla ya kumbukumbu ya miaka minne tangu Urusi ilipoivamia Ukraine Februari 24 mwaka 2022. Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas amesema mazungumzo ya Brussels yatalenga kuishinikiza zaidi Urusi.Trump kukutana uso kwa uso na Putin

''Bila shaka tunamajadiliano kuhusu Ukraine, kwahivyo ni wazi tutajadili kuhusu awamu ya 20 ya vikwazo lakini kama mnavyojuwa nyote, nafikiri hakutakuwa na hatua kubwa itakayopigwa leo kuhusiana na hili. Lakini bila shaka tutashinikiza suala hilo.''

Hungary imetishia mwishoni mwa Juma kuzuia mipango yote ya kuiwekea vikwazo Urusi  na kuipatia mkopo wa yuro bilioni 90 Ukraine hadi pale usafirishaji wa mafuta kutoka Urusi kwenda Hungary utakaporuhusiwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW