1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

EU yaandaa mkopo wa euro bilioni 90 kwa Ukraine

1 Aprili 2026

Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, imeandaa msingi wa sheria wa kujaribu kutoa awamu ya kwanza ya mkopo wa euro bilioni 90 kwa Ukraine inayokabiliana na mashambulizi kutoka Urusi.

Australien Canberra 2026 | Ursula von der Leyen spricht vor dem australischen Parlament
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der LeyenPicha: Lukas Coch/AAP/dpa/picture alliance

Fedha hizo bado zimekwama kufuatia upinzani wa Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban ambaye ni rafiki wa karibu wa rais wa Urusi Vladimir Putin.

Rais wa Halmashauri hiyo Ursula von der Leyen, amesema mkopo huo utafanikiwa kutolewa licha ya pingamizi hilo. Amesema hatua hiyo inatoa ujumbe wa wazi kabisa kwamba Ulaya iko tayari kusonga mbele.

Halmashauri hiyo imeandaa mswada wa kupitisha fedha hizo ambao unahitaji idhini ya pamoja ya nchi zote 27 za EU ili mkopo huo uanze kutolewa.

Chini ya mpango huo dola bilioni 45 zinazotarajiwa kutolewa mwaka 2026, dola bilioni 16.7 zinalenga kusaidia katika masuala ya bajeti ya Ukraine na dola bilioni 28.3 zikilenga kuimarisha sekta yake ya ulinzi pamoja na uwezo wake ikijumuisha utengenezaji wa droni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW