1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

EU yahimiza usitishaji wa vita vya Israel na Hezbollah

24 Novemba 2024

Mwanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, ametoa wito wa kusitisha vita kati ya Israel na Hezbollah wakati wa ziara yake nchini Lebanon.

Umoja wa Ulaya wahimiza usitishaji mara moja wa vita vya Israel na Hezbollah
Umoja wa Ulaya wahimiza usitishaji mara moja wa vita vya Israel na HezbollahPicha: European Union

Mashambulizi ya anga ya Israeli dhidi ya jeshi la Lebanon yameua mwanajeshi mmoja na kujeruhi wengine 18, huku Hezbollah ikijibu kwa kurusha maroketi ndani ya Israel.

Katika Ukanda wa Gaza, Israeli imewataka wakaazi wa vitongozi vya mashariki mwa Ukanda huo kuhama, na kusababisha wimbi jipya la watu kuyahama makaazi yao, huku shambulizi la droni likiripotiwa kumjeruhi mkurugenzi wa hospitali ya Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW