EU yaidhinisha makubaliano ya kudhibiti wahamiaji
14 Mei 2024Matangazo
Hatua hiyo ni katika wakati ambapo kampeni za uchaguzi wa bunge la Ulaya utakaofanyika mwezi ujao, zimepamba moto. Suala la uhamiaji linatarajiwa kuchukuwa sehemu kubwa ya kampeini za uchaguzi huo. Makubaliano hayo mapya ya Uhamiaji yameidhinishwa rasmi na mawaziri wa uchumi wa mataifa 27 wanachama na kumaliza zaidi ya miaka 8 ya mchakato wa kuyaandaa. Makubaliano hayo yatasimamia mfumo wa kuwashughulikia watu wanaoingia Ulaya kinyume cha sheria.Hungary na Poland ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikipinga utaratibu wa aina yoyote wa kulazimisha nchi kuwapokea wahamiaji au kutowa fedha kwaajili ya wahamiaji hao,zimepiga kura ya kuyapinga makubaliano hayo.