1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

EU yaitaka Venezuela kusitisha ukandamizaji wa upinzani

8 Septemba 2024

Umoja wa Ulaya unaitaka Venezuela kukomesha ukandamizaji wake dhidi ya viongozi wa upinzani na kuwaachia huru wafungwa wote wa kisiasa. Haya yamesemwa leo na mkuu wa sera za nje wa Umoja huo, Josep Borrell.

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell wakati wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels mnamo Agosti 29,2024
Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya - Josep BorrellPicha: Francois Lenoir/European Union

Haya yanajiri wakati ambapo mgombea urais wa upinzani wa Venezuela, Edmundo Gonzalez, ameondoka nchini humo kuelekea Uhispania usiku wa kuamkia leo kutafuta hifadhi. Haya yamesemwa na maafisa nchini humo wakati kuna ongezeko la mzozo wa kisiasa na kidiplomasia juu ya matokeo tata ya uchaguzi wa Julai.

Soma pia:Venezuela imewafungwa mamia kwenye jela zenye ulinzi mkali baada ya uchaguzi

Kuondoka kwa Gonzalez mwenye umri wa miaka 75 nchini Venezuela, ambaye Marekani, Umoja wa Ulaya na mataifa mengine yenye ushawishi yanamuona kama mshindi halali wa uchaguzi huo, kunakuja wiki moja baada ya mamlaka yaVenezuela kutoa waranti ya kukamatwa kwake, ikimshtumu kwa kupanga njama dhidi ya serikali pamoja na uhalifu mwingine.