1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yajadili Brexit, wakimbizi na ulinzi

22 Juni 2017

Viongozi wakuu wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels kwenye mkutano wa kilele kujadili hatua za mwisho mwisho za Uingereza kujiondoa kutoka Umoja huo, na masuala tete ya wakimbizi na sera ya ulinzi.

Europaparlament in Straßburg
Picha: picture-alliance/Winfried Rothermel

Ni jambo lisilokanushika kwamba hali imechangamka: mwenyeji wa mkutano huo wa kilele na rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk tayari anaitaja hali kama ni "kurudi kwenye Umoja wa Ulaya ni ufumbuzi na sio tatizo."

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ameridhishwa na matokeo ya uchaguzi nchini Uholanzi na Ufaransa, akiamini kwamba Ulaya inaweza kusonga nbele. Hata hivyo, anasema lazima kuchukuliwe hatua za kuunawirisha Umoja wa Ulaya licha ya kwamba hali kwa jumla sio nzuri hivyo. Anasema Merkel kuwa "Umoja wa Ulaya uko katika hali ngumu."

Wasiwasi wa Kansela Merkel kwa kiasi kikubwa unatokana na kujitowa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May, atapata fursa ya kuzungumza kwa dakika chache wakati wa chakula cha usiku kuhusu kujitowa kwa Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya.

Kwa muda mrefu, Merkel alikuwa hataki kwa makusudi kukabiliana na suala hilo ambapo anasema: "Hatari ya mazungumzo ya kujitowa kwa Uingereza ni kwamba hatujali sana juu ya mustakbali wetu."

Tubakie pamoja 

Maafisa wa idara mbili muhimu kwenye Umoja wa Ulaya - Benki ya Umoja wa Ulaya na Mamlaka ya Usimamizi wa Madawa - lazima waondoke nchini Uingereza. Ujerumani ingelipenda kuwapatia makaazi mapya mamlaka hizo zote mbili. Lakini nchi nyengine nyingi pia zinataka kufanya hivyo na tayari kumezuka mzozo wa kuziteuwa.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na waziri wake wa mambo ya nje Sigmar Gabriel.Picha: picture-alliance/dpa/B. von Jutrczenka

Kwa upande wa Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Donald Tusk, na kwa serikali ya Ujerumani, zote, zinashinikiza kufikiwa kwa makubaliano ya haraka. Wito wa Merkel kwa hilo ni mfupi kwamba: "Tubakie pamoja."

Hata hivyo, suala hilo la kuendelea kubakia pamoja haliwezi kutajwa hususan linapokuja suala la wakimbizi. Mfumo wa kutafuta hifadhi wa Umoja wa Ulaya tayari umehamia katika hatima isiojulikana.

"Hali katika njia ya Bahari ya Mediterenia inazidi kuwa mbaya," wanalalamika maafisa wa Umoja wa Ulaya.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Austria, Sebastian Kurz, angelipenda kufungwa kwa njia ya Libya kukimbilia Italia na kujenga kambi ya wakimbizi nchini Libya na ni  Hungary pekee ndiyo hadi sasa iliyoridhia hilo.

Halafu kuna suala la ulinzi. Kujitowa kwa Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya na taathira ya uongozi wa Trump, kunaufanya Umoja wa Ulaya kuwa nna shauku ya kumarisha ulinzi wake.

"Hatuwezi tena kutegemea msaada wa nje kwa ulinzi wa Ulaya," anasema hayo Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya, Jean-Claude Juncker.

Mkutao huo wa kilele unataka kuonyesha kuanza ulinzi shirikishi. Hata hivyo, suala la umoja wa kweli ndani ya Umoja wa Ulaya wenyewe litaendelea kubakia kuwa jambo muhimu kuliko yote.


Mwandishi: Kai Küstner
Tafsiri: Mohamed Dahman
Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW