1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamhuri ya Moldova

EU yampongeza Maia Sandu kwa ushindi wa urais, Moldova

4 Novemba 2024

Rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, leo amempongeza Rais wa Modova Maia Sandu kwa kuchaguliwa tena kama rais wa nchi hiyo na kwa mustakabali wa Ulaya wa taifa hilo.

Rais wa Moldova Maia Sandu akiwahutubia waandishi wa habari baada ya kufungwa kwa kura za maoni kwa ajili ya uchaguzi wa rais
Rais wa Moldova Maia SanduPicha: Vadim Ghirda/AP/dpa/picture alliance

Katika ujumbe alioandika kwenye mtandao wa kijamii wa X, von der Leyen, amemwambia rais huyo kwamba kunahitajika ukakamavu wa kipekee kukabiliana na changamoto alizokumbana nazo katika uchaguzi huo.

Moldova yapiga kura katika uchaguzi tete kuhusu mustakabali wa EU

von der Leyen pia ameelezea furaha ya kuendelea kushirikiana na rais Sandu kuelekea mustakabali wa Ulaya kwa Moldova na watu wake.

Moldova iliingia katika duru ya pili ya uchaguzi

Ushindi wa Sandu unakuja baada ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais jana Jumapili.

RaisSandu, alipata asilimia 42.5 katika duru ya kwanza, huku Alexandr Stoianoglo, anayeungwa mkono na Urusi, akipata asilimia 26.