1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

EU yamrejesha nyumbani balozi wake Niger

Saleh Mwanamilongo
24 Novemba 2024

Idara ya kidiplomasia ya EU imesema kulikuwa na "tofauti kubwa" juu ya shutuma zilizotolewa na viongozi wa kijeshi wa Niger.

EU yamrejesha nyumbani balozi wake Niger kufuatia mzozo kuhusu msaada wa kiutu
EU yamrejesha nyumbani balozi wake Niger kufuatia mzozo kuhusu msaada wa kiutuPicha: Denis Doyle/Getty Images

Ijumaa, wizara ya Mambo ya Nje ya Niger iliushutumu Umoja wa Ulaya kwa kutenga dola milioni 1.3 katika misaada ya kibinadamu kwa mashirika kama vile Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na Baraza la Wakimbizi la Danmark bila kushauriana na mamlaka. Viongozi wa Niger walisema hatua hiyo haikuzingatia kanuni za uwazi na ushirikano mzuri baina ya pande mbili.

Kwa upande wake EU iliwashutumu viongozi wa Niger kutumia misaada ya kibinadamu kwa malengo ya kisiasa. Fedha hizo ni msaada uliotakiwa kuelekezwa kwa waathirika wa mafuriko makubwa yaliyoikumba nchi hiyo ya Sahel.