EU yamuwekea vikwazo kiongozi wa kijeshi wa RSF
21 Novemba 2025
Matangazo
Mateso hayo yanajumuishamashambulizi yanayofanywa na kundi hilo katika mji wa El Fasher ulio magharibi mwa mkoa wa Darfur, uliodhibitiwa hivi karibuni na kundi hilo la RSF, baada ya kuzingirwa kwa miezi 18.
Vikwazo hivyo dhidi ya Abdel-Rahim Hamdan Dagalo vinafuatia vikwazo sawa na hivyo vilivyotolewa kwa kaka yake ambae ni kiongozi wa kundi RSF linalopambana na jeshi la Sudan, Mohamed Hamdan Dagalo.
Baraza la masuala ya nje la Umoja wa Ulaya, limesema limemuwekea vikwazo Abdel-Rahim, kufuatia ukiukwaji wa haki za binaadamu uliofanywa na vikosi vyake katika mji wa El Fasher, Sudan