1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yaongeza watu tisa katika orodha yake ya vikwazo

26 Julai 2024

Umoja wa Ulaya umewaongeza watu tisa na muungano mmoja wa waasi kwenye orodha yake ya vikwazo dhidi ya makundi yenye silaha yanayochochea mzozo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Umoja wa Ulaya
EU yaongeza watu tisa katika orodha yake ya vikwazoPicha: James Arthur Gekiere/Belga/dpa/picture alliance

Hatua hiyo inawalenga makamanda kadhaa wa makundi kadhaa na muungano unaoitwa Muungano wa Mto Kongo, na kufanya hesabu jumla ya walioingia kwenye orodha ya vikwazo vyake kwa ajili ya Kongo kufikia 31.

UN yawawekea vikwazo waasi wa Kongo huku mapigano yakiendelea

Katika taarifa, Baraza la Umoja wa Ulaya limesema kuwa walioorodheshwa walishutumiwa kwa vitendo vinavyojumuisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kwa kuendeleza migogoro ya silaha, ukosefu wa utulivu na usalama Mashariki mwa nchi hiyo.

Kuorodheshwa kwa Muungano wa Mto Kongo unaojulikana kwa jina la Kifaransa kama Alliance Fleuve Congo", ama  AFC, kunakuja siku moja baada ya Marekani pia kuuwekea vikwazo muungano huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW