1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU: Yapendekeza pasi maalum ya chanjo ya virusi vya corona

1 Machi 2021

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen amesema atapendekeza sheria za pasi ya chanjo ya Umoja wa Ulaya mwezi huu, wakati kanda hiyo ikijiandaa kuimarisha kampeni za chanjo.

Symbolbild Immunitätspass
Picha: Axel Bueckert/Zoonar/picture alliance

Von der Leyen amesema katika ujumbe wa Twitter kuwa pasi hiyo ya kidigitali ya kijani, italenga kutoa uthibitisho wa kuchanjwa na matokeo ya vipimo vya covid-19.

Pasi hiyo itawaruhusu watu kutembea kwa usalama katika nchi za Umoja wa Ulaya au nje kwa ajili ya kazi au utalii.

Katika mkutano mwingine na wabunge wa Ujerumani katika bunge la shirikisho na wale wa Bunge la Ulaya, von der Leyen amesema Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya itaanzisha cheti maalum cha kidijitali katika miezi ijayo kitakachokubalika na nchi 27 wanachama wa umoja huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW