1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaYemen

EU ´yapiga jeki´ mashirika yanayotoa msaada Yemen

8 Mei 2024

Umoja wa Ulaya umetangaza msaada wa dola milioni 125 kuyapiga jeki mashirika ya Umoja wa Mataifa na yale yasiyo ya kiserikali yanayowasaidia watu nchini Yemen.

Baa la njaa|Yemen
Ukosefu wa chakula unayakumba maeneo mengi nchini Yemen. Picha: Mohammed Hamoud/AA/picture alliance

Tangazo la msaada huo limetolea mjini Brussels siku moja baada ya makundi ya misaada ya kiutu kuurai ulimwengu kuchangia mabilioni ya fedha ili kuwezesha misaada muhimu kuifikia Yemen.

Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya imesema kitita hicho cha fedha kitatumika kuwasaidia wale "walio na uhitaji mkubwa zaidi".

Mnamo Jumatatu mashirika ya hisani yaliiyoomba jumuiya ya kimataifa kuchangisha alau dola bilioni 2.3 za msaada kwa Yemen, taifa lililoharibiwa na muongo mmoja wa vita.

Inakadiriwa zaidi ya watu milioni 34 nchini humo wanahitaji msaada wa kibinadamu ikiwemo chakula na dawa.