EU yasema vitisho havitakubaliwa kama hali ya kawaida
14 Novemba 2025
Matangazo
Baada ya mkutano na mawaziri wa ulinzi wa Ujerumani, Ufaransa, Italia, Uingereza na Poland, Kallas amewaambia waandishi wa habari mjini Berlin kwamba Umoja huo wa Ulaya hauwezi kukubali vitisho hivyo kama hali mpya ya kawaida.
Uhamishaji wa wanajeshi na vifaa utahusisha wanachama wa EU
Pia amesema mpango wa uhamishaji wa vifaa na wanajeshi wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya utajumuisha kuunganisha rasilimali za usafiri za nchi wanachama na mapendekezo ya kuharakisha michakato ya kupatikana kwa vibali vya usafiri.