1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yasisitiza kuimarisha mpango wa mageuzi ya Palestina

21 Novemba 2025

Umoja wa Ulaya umesisitiza kuimarisha mpango wa mageuzi wa mamlaka ya Palestina, wakati wajumbe 60 wa Ulaya wakikutana Brussels kujadili ujenzi na uongozi mpya wa Ukanda wa Gaza.

Ubelgiji Brüssel 2025 | Wajumbe 60 wa Ulaya wajadili mpango wa mageuzi wa mamlaka ya Palestina
EU yasisitiza kuimarisha mpango wa mageuzi wa mamlaka ya PalestinaPicha: Alexandros Michailidis/European Union

Tamko lao limejiri baada ya kupitishwa mpango wa amani wa Ukanda huo uliosimamiwa na Marekani.

Umoja huo wenye nchi wanachama 27 na unaochangia pakubwa kifedha kwa mamlaka ya Palestina, unajaribu kuchukua jukumu muhimu baada ya kuwekwa kando katika juhudi za rais wa Marekani Donald Trump kumaliza vita vya Israel na Hamas.

Kamishna wa Umoja wa ulaya anayehusika na nchi za kanda ya bahari ya Meditterania Dubravka Suica, amesema nia yao ni kuimarisha uongozi katika Ukanda wa Gaza, Kujenga uchumi imara na kuimarisha huduma kwa watu wa eneo hilo pamoja na kuweka mazingira mazuri kwa serikali ijayo.

Mamlaka ya Palestina, ambayo inasimamia baadhi ya maeneo yanayojitawala kwa kiasi fulani katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel, inafanya juhudi mpya za kuwa mhusika katika Gaza ya baada ya vita.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW