1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yatishia kujibu vikwazo vya Marekani kwa raia wa Ulaya

24 Desemba 2025

Tume ya Ulaya imetishia kuchukua hatua za kujibu baada ya Marekani kuwawekea vikwazo raia watano wa Ulaya kwa madai ya kuhusika na udhibiti wa majukwaa ya mtandaoni ya Marekani.

Brussel 2025 | Antonio Costa
Tume ya Ulaya imesema italazimika kuchukua hatua za haraka na madhubuti kulinda uhuru wa kisheria dhidi ya hatua zisizo na msingi.Picha: Stephanie Lecocq/REUTERS

Mkuu wa Umoja wa Ulaya Antonio Costa amelaani vikali marufuku ya kuingia Marekani iliyowekwa, akisisitiza kuwa haikubaliki kati ya washirika, wadau na marafiki na ameiomba Marekani kutoa ufafanuzi.

Katika taarifa yake,Tume hiyo imesema ililazimika itachukua hatua za haraka na madhubuti kulinda uhuru wa kisheria dhidi ya hatua zisizo na msingi.

Hata hivyo haikuwekwa wazi ni hatua gani inaweza kuchukua endapo mzozo huo utazidi kuongezeka. Huenda inaweza kupendekeza kupunguza ushirikiano na Marekani katika maeneo fulani, au hata kuchukua hatua za kiuchumi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW