1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yazionya nchi zake zijiandae kwa wimbi la homa ya nyani

16 Agosti 2024

Shirika la afya la Umoja wa Ulaya limezitaka nchi wanachama wake zijiandae kwa uwezekano wa wagonjwa zaidi wa virusi vya homa ya nyani.

FILE PHOTO: Illustration shows test tubes labelled "Monkeypox virus positive and negative"
Picha: Dado Ruvic/REUTERS

Hii ni baada ya Sweden kutangaza mgonjwa wa kwanza mwenye virusi vya homa ya nyani.

Kituo cha Ulaya cha kuzuia na kudhibiti magonjwa ECDC kimesema hali ya hatari ndani ya Umoja wa Ulaya bado iko chini.

Kituo hicho hata hivyo kimetoa mwito kwa mamlaka za afya umma ndani ya Umoja huo kuwa macho na kuuhamasisha umma juu ya ugonjwa huo.

Mkurugenzi wa kituo hicho cha ECDC Pamela Rendi-Wagner amesema katika taarifa kuwa, Ulaya inapaswa kujiandaa kwa wagonjwa zaidi hasa aina mpya ya virusi vya homa ya nyani vya clade 1.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW