1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Euro 2022 kwa wanawake yatinga nusu fainali

25 Julai 2022

England watakabana koo na Sweden nao Ujerumani wataangushana na Ufaransa kusaka tiketi ya kucheza katika fainali ya Jumapili ijayo dimbani Wembley na ambayo tiketi zote za mtannage huo zimeuzwa.

EURO 2022 | Frauenfußball
Picha: picture alliance

Mashindano ya Kombe la mataifa ya Ulaya ya Euro 2022 kwa upande wa wanawake yambapo wenyeji England watakabana koo na Sweden nao Ujerumani wataangushana na Ufaransa kusaka tiketi ya kucheza katika fainali ya Jumapili ijayo dimbani Wembley na ambayo tiketi zote za mtannage huo zimeuzwa.

Soma zaidi: Ufaransa yatinga nusu fainali EURO 2022

England watakuwa na mashabiki karibu 30,000 katika mechi yao ya kesho ya nusu fainali na kwa mara ya kwanza katika Euro 2022, wenyeji wa mashindano hayo wanakutana na timu inayoorodheshwa nafasi ya juu kuwaliko katika viwango vya FIFA na hata yenye uzoefu zaidi katika hatua za mwisho mwisho za mashindano makubwa. Kiungo wa England Fran Kirby anatumai kocha mkuu Sarina Wiegman ataisaidia timu hiyo kuivunja laana ya kutoweza kupita katika nusu fainali. "bila shaka kipo akilini mwa baadhi ya wenzangu ambao wamekuwa hapa, nimekuwa katika nusu fainali nne sasa. lakini kwetu ni kuhusu wakati huu na ni kuhusu tunachoweza kufanya ili kuhakikisha kuwa hatuko katika hali hiyo tena."

Sweden ina kibarua kikali dhidi ya EnglandPicha: Naomi Baker/Getty Images

Kocha wa Swden Peter Gerhardsson anasema watajiandaa vikali kuwakabili England. "Tunapozungumzia England ni mambo ya ufundi ambayo wana uzoefu nayo sasa. tutakuwa na mpango. Sijui hasa kwa sasa utakavyofanya kazi. Lakini naweza kukuhakishieni tutakuwa na mpango. Na tunahitaji mpango mzuri. na tunahitaji mpango mzuri. Labda tunahitaji mpango mzuri zaidi."

Soma pia: Sweden yatinga nusu fainali kandanda la wanawake Ulaya

Ujerumani ndio timu yenye mwendelezo mzuriZaidi katika mashindano hayo mpaka sasa. Wameshinda mechi zao zote nne bila kufungwa bao hata moja. Kiungo wa Ujerumani Sara Dabritz ameahidi kuwa watacheza asilimia 100 katika nusu fainali ya Jumatano.

Huwa vigumu sana kwa Ufaransa kwa sababu hadi sasa wamekuwa wakiondolewa katika robo fainali. kwa hiyo kwao ni kitu cha kihistoria na maalum kutinga nusu fainali. Kwa hiyo watakuwa na motisha kubwa na litakuwa pia lengo lao kutinga fainali. Lakini watapambana na Ujerumani yenye motisha kubwa na lengo kubwa na ndoto ya kufika fainali.

Wapinzani wao Ufaransa wameweka historia ya kutinga nusu fainali kwa mara ya kwanza katika mashindano ya Euro kwa wanawake. Mshambuliaji wa Ufaransa Kadidiatou Diani anazungumzia mapungufu ya Ujerumani

"kwangu mimi, mapungufu yao....ndiyo, ni vigumu sana kusema ni mapungufu gani wanayo lakini kwa kweli yapo baadhi. hicho ndicho tutajaribu kukifanyia kazi kwa kutizama video na makocha wetu.

afp, dpa, reuters, ap

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW