1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EURO 2024: Nagelsmann akiandaa kikosi chake

30 Mei 2024

Nahodha wa Ujerumani Ilkay Gündogan na Mabingwa wa Bundesliga Florian Wirtz, Robert Andrich na Jonathan Tah wa Bayer Leverkusen wamefanya mazoezi na kikosi cha Ujerumani.

Julian Naglesmann
Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Julian Naglesmann akiandaa kikosi kwa mechi za Euro 2024.Picha: Alexander Hassenstein/Getty Images

Mara ya kwanza baada ya kuwasili katika kambi ya mafunzo katika jimbo la mashariki mwa Ujerumani la Thuringia.

Wachezaji hao wanne waliwasili siku ya Jumatano, muda mfupi baadaye kuliko wachezaji wengine wote kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani. Wachezaji hao watatu wa Leverkusen walishinda taji la Kombe la UjerumaniJumamosi, huku Gündogan akicheza mechi ya mwisho ya La Liga msimu huu na Barcelona siku ya Jumapili.

Kocha Julian Nagelsmann alikuwa na wachezaji 24 katika kambi ya mazoezi kufikia Alhamisi, ambapo mazoezi yalifanywa katika vikundi viwili huku mvua ikiwanyeshea wachezaji.

Soma pia:Ujerumani yaipiga Uholanzi 2 - 1 mechi ya kirafiki

Mcheza kwao hutuzwa

Picha: Jan Huebner /Imago Images

Huku Ujerumani ikijiandaa kwa mashindano ya kombe la Euro 2024 katika ardhi ya nyumbani, wachezaji wa timu ya taifa pia wanapaswa kutayarishwa kukabiliana na hali ya hatari kwa kupata mafunzo kutoka kwa kikosi kazi maalum cha polisi.

Wachezaji watano bado hawajajiunga na kambi ya mazoezi. Wawili wa Borussia Dortmund

Niklas Füllkrug na Nico Schlotterbeck na wachezaji wa Real Madrid Toni Kroos na Antonio Rüdiger ambao watacheza fainali ya Ligi ya Mabingwa siku ya Jumamosi mjini London, huku kipa wa Barcelona Marc-André ter Stegen akitarajiwa kuwasili Jumatatu.

Kikosi cha Nagelsmann kitaondoka Blankenhain kuelekea katika kambi yao Herzogenaurach siku ya Ijumaa, kabla ya mechi ya Ukraine huku mtihani wa mwisho ni Juni 7 dhidi ya Ugiriki.

Ujerumani itafungua dimba la mashindano ya Euro 2024 dhidi ya Scotland mnamo Juni 14. Kabla ya kumenyana na Hungary na Uswizi katika hatua ya makundi wakati wakitarajia kufikia fainali itakayoandaliwa mjini Berlin Julai 14.