1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EURO 2024: Slovakia yalenga "kuipiga" England

30 Juni 2024

Kocha wa Slovakia Francesco Calzona anaamini England wana kikosi bora zaidi kwenye michuano ya Euro 2024, kabla ya mechi yao ya 16 bora siku ya Jumapili.

Kandanda-Euro 2024 | England vs. Slovakia |
Mashabiki wa timu ya taiafa ya kandanda ya Slovakia katika uga wa Gelsenkirchen.Picha: Bernadett Szabo/REUTERS

Kikosi cha Gareth Southgate kiliongoza Kundi C licha ya kufunga mabao mawili pekee ushindi wa 1-0 dhidi ya Serbia ukifuatiwa na sare ya dhidi ya Denmark na Slovenia.

Soma pia: EURO 2024: Ujerumani yatinga robo fainali lakini hali bado ni tete

England imepokea shutuma kali kutoka kwa mashabiki na wafuatiliaji kandanda wa nyumbani kwani uchezaji wao umeshindwa kufikia viwango na matarajio ya mashabiki wake.

Hata hivyo kocha Calzona amesisitiza kwamba watajitahidi kukaa kushindwa na kutumia makosa ya England kuiadhibu.

Katika mechi nyengine ya kufuzu kwa raundi ya mtoano, Uhispania itapimana na Georgia katika uga wa Rhein Energie mjini Köln.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW