1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EURO 2024: Unachopaswa kufahamu

7 Juni 2024

Mashindano ya ubingwa wa Ulaya EURO 2024 kwa wanaume ndio tamasha kubwa kabisa la michezo kuandaliwa Ujerumani tangu Kombe la Dunia la FIFA mwaka wa 2006. Kina nani wanapigiwa upatu? Mechi zitachezwa wapi?

Euro 2024
Albärt ndiye atakayetumika kama kibonzo cha utambulisho wa mashindano ya Euro 2024 nchini UjerumaniPicha: Arne Dedert/dpa/picture alliance

Nani wanapigiwa upatu?

Wabashiri wa matokeo ya michezo wamewaweka makamu bingwa wa Euro 2020 England mbele ya makamu bingwa wa Kombe la Dunia Ufaransa na wenyeji Ujerumani. Mabingwa watetezi Ujerumani wako katika nafasi ya sita kwenye ubashiri wa matokeo.

Albania, Slovakia na wageni katika mashindano ya Ulaya Georgia zinaonekana kupewa nafasi kama timu zinazoweza kuwashangaza wengi kwa kufanya vyema.

Kwa kuzingatia orodha ya viwango vya kimataifa vya FIFA, taji linapaswa Kwenda kwa Ufaransa, ambao wako nafasi pili nyuma ya mabingwa wa dunia Argentina. Ubelgiji wako katika nafasi ya tatu, England nafasi ya nne na Ureno ya sita. Ujerumani wako nafasi ya 16 na kwa sasa ndio timu bora ya tisa Ulaya kwa mujibu wa orodha hiyo.

Muundo gani utatumika?

Ujerumani itamudu kufanya maajabu Kombe la Euro 2024?

01:29

This browser does not support the video element.

Muundo wa kinyang'anyiro hicho ni sawa na mashindano mawili ya mwisho ya Euro, huku timu 24 zikishiriki. Awali, timu nne zitakabana koo kila mmoja katika makundi sita. Washindi wa makundi na watakaomaliza wa pili, pamoja na timu nne zitakazomaliza katika nafasi ya tatu, zitafuzu katika duru ya 16. Kama timu katika kundi moja zitakuwa na pointi sawa, kigezo kitakachozingatiwa cha kwanza ni matokeo ya mechi za nyumbani na ugenini kati ya timu hizo mbili.

kama timu mbili bora za nafasi ya tatu katika makundi tofauti zitakuwa zimetoshana pointi, tofauti ya mabao itazingatiwa.

Mfumo wa mtoano kisha utaendelea mpaka robo fainali na nusu fainali hadi fainali. Kama hapatakuwa na mshindi katika dakika 90, mechi za mtoano huamuliwa na vipindi viwili vya muda wa ziada wa dakika 15 kila kipindi au mikwaju ya penalti.

Mechi zitachezwa wapi?

Kuna jumla ya viwanja 10 vitakavyotumika kwa mechi 51. Olympiastadion mjini Berlin (watazamaji 71,000), Munich (66,000) na Dortmund (62,000) vitatumiwa kwa mechi nyingi, ambazo ni sita. Berlin, uwanja mkubwa zaidi kati ya hivyo 10, utakuwa na robo fainali moja. Mechi moja ya duru ya 16 na mechi tatu za makundi pamoja na fainali ya Julai 14. Euro 2024 inafungua pazia Juni 14 mjini Munich kwa mtanange kati ya Ujerumani na Scotland.

Eneo la mashabiki la Lango la Brandenburg zinaweza kuwa na watazamani 30.000Picha: Geisler-Fotopress/picture-alliance

Viwanja mjini Stuttgart (51,000), Hamburg (49,000), Düsseldorf (47,000), Frankfurt (47,000) na Cologne (43,000) vitakuwa na mechi tano katika kila uwanja. Leipzig (40,000) na Gelsenkirchen (50,000) vitatumika kwa mechi nne kila uwanja. Düsseldorf ni mji pekee ambao haukuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la Wanaume 2006. Nuremberg, Hanover na Kaiserslautern havikupata nafasi mara hii.

Mashabiki wanaweza kutizama mechi wapi nje ya viwanja?

Kutakuwa na maeneo maalum ya mashabiki katika miji yote wenyeji, ambao mechi zitaoneshwa kwenye skrini kubwa. Kuingia katika maeneo hayo ya mashabiki na maeneo mengine ya umma ya kutizama mechi ni bila malipo. Kama ilivyokuwa wakati wa Kombe la Dunia la 2006, makumi kwa maelfu ya mashabiki wa kandanda wanatarajiwa kukusanyika katika Lango maarufu la Brandeburg mjini Berlin, Bustani ya Olimpiki mjini Munich na kwenye kingo za Mto Main mjini Frankfurt kutizama mechi Pamoja.

Hali ya usalama ikoje?

"Usalama wa mashindano ya kandanda la Ulaya nchini mwetu ni suala la kipaumbele," alisema Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Nancy Faeser. "Polisi watawekwa katika viwanja vyote vya michezo na kila sehemu zitakazokuwa na idadi kubwa ya watu."
Ukaguzi wa mipakani umepangwa wakati wa mashindano hayo. Zaidi ya yote, maafisa wa usalama wanalenga kuwazuia magaidi na wahuni kuingia Ujerumani. Serikali ya Uingereza, kwa mfano, imewawekea marufuku ya kutoka nchini mashabiki 1,600 wanaoonekana kusababisha vurugu kwa kipindi kizima cha mashindano ya Ulaya.

Polisi ya Ujerumani, inayohusika na mipaka, itakuwa na karibu maafisa 22,000 kote nchini watakokuwa zamu kila siku. Watasaidiwa na mamia kadhaa ya maafisa wenzao kutoka nje ya Ujerumani.

Ushirikiano na vikosi vya usalama vya Ufaransa utakuwa wa karibu sana – pia kutokana na matamasha mawili makubwa ya michezo mjini Paris baada ya mashindano ya Ulaya – Michezo ya Olimpiki (Julai 26 hadi Agosti 11) na Michezo ya Olimpiki kwa Walemavu (Agosti 28 hadi Septemba 8).

Makala hii kwanza ilichapishwa katika Kijerumani.

Polisi watawekwa katika viwanja vyote vya michezo na kila sehemu zitakazokuwa na idadi kubwa ya watu.Picha: Daniel Kubirski/picture-alliance
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW