1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Evian:Nchi tano za Ulaya kupambana na uhamiaji haramu

6 Julai 2005

Nchi tano muhimu katika Jumuiya ya Ulaya zimekubaliana kushirikiana kuzuwia uhamiaji usiokuwa wa kisheria katika nchi hizo. Baada ya kukutana katika mji wa Evian, mwenyeji ambaye ni waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, amesema Ufaransa, Spain na Italy zitafanya doria katika Bahari ya Mediterranean kuzuwia mashua zinazotokea nchi za Afrika ya Kaskazini. Spain na Ufaransa pia zimetoa wa kutumiwa safari za ndege za pamoja kuwarejesha makwao wahamiaji haramu. Nchi hizo tano, zikiwemo pia Ujerumani na Uengereza, pia zimekubaliana juu ya kuingizwa alama za vidole katika paspoti.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW