Wataalamu wa UN wanashughulikia ripoti ya mazingira
2 Desemba 2025
Wanaketi kikao hicho huku makubaliano ya kimataifa kuhusu ongezeko la joto duniani yakikabiliwa na changamoto kutoka kwa Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye anadai sayansi hiyo ni "udanganyifu”. Waziri wa Ikolojia wa Ufaransa, Monique Barbut, ambaye nchi yake inakaribisha mkutano wa siku tano katika kitongoji cha Paris, aliwaambia wanasayansi kuwa kazi yao "ya thamani kubwa sana” ni muhimu wakati ushirikiano wa kimataifa umedhoofika. Kadhalika alisema kuna jambo lingine pia ambalo linapaswa kuwatia wasiwasi wote ambalo ni kuongezeka kwa upotoshaji kuhusu hali ya hewa kwenye mitandao ya kijamii, magazeti na hata ndani ya taasisi za kisiasa.Kazi wataalamu hao inakabiliwa na vikwazo kutokana na utawala wa Marekani, ambapo rais aliita mabadiliko ya tabianchi ‘udanganyifu mkubwa zaidi' na ‘hoax' wakati wa hotuba katika Umoja wa Mataifa mwezi Septemba.