Ujerumani ipo tayari kuingilia mvutano wa Serbia na Kosovo
3 Oktoba 2023Matangazo
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Boris Pistorius amesema taifa lake linafuatilia kwa karibu hali ya mvutano unaoendelea kati ya Serbia na Kosovo na kwamba watachukua hatua pale itakapolazimika.Ametoa wito wa kurejeshwa kwa hali ya utulivu, hata hivyo hakuondosha uwezekano wa kuongezwa kwa wanajeshi wa Ujerumani katika mpango wa amani unaoongozwa na NATO, kama ilivyofanywa na Uingereza, ingawa pia ameongeza kuwa kwa sasa bado hakujawa na mpango huo.Awali mwenyekiti wa kamati ya ulinzi katika bunge la Ujerumani, Marie-Agnes Strack-Zimmermann alitoa wazo la kupelekwa wanajeshi zaidi katika mpango huo wa amani ujulikano kama KFOR.Kwa sasa kuna takribani wanajeshi 85 wa Ujerumani katika mpango huo unaoongozwa na Jumuiya ya Kujihami ya NATO.