1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

F1: Hamilton ashinda taji la dunia kwa mara ya sita

Bruce Amani
4 Novemba 2019

Mmoja baada ya mwingine, Lewis Hamilton amewapiku madereva bora zaidi wa Formula One. Isipokuwa mmoja tu. Na sasa Hamilton anaikaribia kwa kasi historia ya dereva bora Michael Schumacher.

Formel 1 | Grand Prix USA
Picha: Getty Images/AFP/M. Thompson

Nafasi zake za kumkamata, wakati mmoja ilidhaniwa kutowezekana, lakini sasa, zinaoenaka kuwa nzuri kabisa.

Dereva huyo wa timu ya Mercedes alishinda ubingwa wake wa sita wa F1 jana alipomaliza katika nafasi ya pili ya mashindano ya US Grand Prix, na kumuacha na tofauti ya taji moja tu akifikisha saba aliyoyashinda Schumacher katika mafanikio ya Mjerumani huyo kati yam waka wa 1994 na 2004.

Muingereza Hamilton amempiku Muargentina Juan Manuel Fangio aliyeshinda mataji matano katika miaka ya 1950. Hamilton sasa anasimama peke yake nyuma ya Schumacher.

Ijapokuwa Hamilton alisema huenda akabaki na timu yake ya Mercedes baada ya kandarasi yake ya sasa kukamilika 2020, ana umri wa miaka 34 na ni mmoja wa madereva wa uzeofu mubwa katika mashindano hayo. Dereva mwenza wa Hamilton, Vakteri Bottas alishinda mbio za jana za Texas, huku Max Verstappen akipanda jukwaani katika nafasi ya tatu