1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

F1: Perez awapiku Ferrari na kushinda Monaco Grand Prix

30 Mei 2022

Dereva wa timu ya Red Bull katika mbio za magari ya Formula One Sergio Perez na kushinda mbio za mkondo wa Monaco. Mashindano hayo yalikumbwa na vurugu kutokana na mvua iliyomwagika

Formel 1 I Sergio Perez gewinnt großen Preis von Monaco
Picha: Christian Bruna/AP/picture alliance

Red Bull ilimnyima dereva Sergio Perez fursa ya kupata ushindi nchini Uhispania kwa kutoa maagizo ya timu ambayo yalimkatisha tamaa nyota huyo wa Mexico.

Huku akihakikishiwa kuwa angeruhusiwa kushindana na kupata ushindi msimu huu, Perez alielekea katika mashindano ya Monaco Grand Prix akiwa bado na mawazo hayo ya Red Bull kichwani. Kisha akapata ushindi wake wa kwanza wa Formula One msimu huu. Ushindi huo hata hivyo haukuja kiurahisi kutokana na mashindano ambayo yalivurugwa na mvua kali.

Ferrari walijikanganya katika maamuzi ya kimkakati na Red Bull wakayatumia makosa hayo kwa faida yao. Charles Leclerc ambaye alikuwa anaongoza mbio hizo za jana alijikuta akimaliza wa nne. Max Verstappen wa Red Bull alimaliza wa tatu huku Carlos Sainz akimaliza wa pili kwa timu ya Ferrari.

Mwisho wa michezo, kwa mengi zaidi tembelea ukurasa wetu wa michezo, kwenye dw.com/kiswahili. Mimi ni Bruce Amani, shukrani kwa kuwa nami

ap

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW