Faeser: Wafuasi wa Hamas wanapaswa kufurushwa Ujerumani
15 Oktoba 2023Matangazo
Faeser amesema watatumia njia zote za kisheria kuwafurusha wafuasi wa Hamas. Matamshi ya Faeser yameungwa mkono na kiongozi wa chama cha Social Democrat (SPD) Lars Klingbell ambaye ameliambia gazeti la shirika la habari la Funke kuwa ikiwa mtu anawaunga mkono Hamas hadharani na hana uraia wa Ujerumani, basi atafukuzwa kutoka nchini.
Kilingbell asema anayepinga maadili ya Ujerumani atanyimwa uraia
Klingbell ameongeza kuwa njia za kisheria zitatumikana na kwamba yeyote anayepinga maadili ya Ujerumani kama kuunga mkono ugaidi na chuki dhidi ya Wayahudi atanyimwa uraia wa Ujerumani.
Marekani, Umoja wa Ulaya, Ujerumani ikiwemo, pamoja na nchi nyingine kadhaa, zimeliweka kundi la Hamas kwenye orodha ya magaidi.