1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fahamu mizani ya kijeshi kati ya Israel na Hamas

23 Oktoba 2023

Majeshi ya Israel hutajwa kuwa na rasilimali au zana bora ulimwenguni huku yakiungwa mkono pakubwa na Marekani, huku uwezo wa kundi la Hamas ukitajwa na wachambuzi kufadhiliwa pakubwa na washirika wake

Vifaru vya Israel vikiwa katika msururu wa pamoja
Vifaru vya Israel vikiwa katika msururu wa pamojaPicha: JALAA MAREY/AFP/Getty Images

Katika vita vya Israel dhidi ya kundi la Hamas, ambalo Marekani na Umoja wa Ulaya zimeliorodhesha kuwa la kigaidi, inakabiliana na kundi lenye silaha na lenye mafunzo ya juu ambalo linaungwa mkono na nchi washirika zenye nguvu katika Ukanda huo. 

Kulingana na taasisi ya Kimataifa ya Mafunzo ya Kimkakatiya Uingereza (IISS), vikosi vya jeshi la Israel vina jumla ya maafisa 169, 500, ambapo 126,000 kati yao ni wanajeshi. 

Zaidi ya hayo, Israel pia ina wanajeshi wa akiba 400,000, ambapo tayari 360,000 wameshaitwa tangu shambulizi la Hamas la Oktoba 7.

Soma pia: Israel yaendeleza mashambulizi Gaza
      
Israel ina baadhi ya mifumo ya kiteknolojia ya kisasa zaidi ya ulinzi ulimwenguni, ukiwemo mfumo wake wa kuzuia makombora “Iron Dome”.

Taasisi ya IISS inasema Israel ina vifaru vya kivita 1,300 na magari mengine maalum ya kivita.

Angani, taasisi hiyo inakadiria Israel kuwa na ndege za kivita 345. Hiyo ikiwa ni kando na ndege zisizohitaji rubani yaani 'drones'.

Nyambizi za kisasa baharini ambazo idadi hazikutajwa ni sehemu ya zana za Israel kivita pamoja na silaha nyinginezo.

Israel inamiliki silaha za nyuklia?

Japo Israel haijaorodheshwa kuwa miongoni mwa nchi zinazomiliki silaha za nyuklia, wachambuzi wanahoji kuwa hifadhi ya silaha za nyuklia za Israeli ni siri iliyo wazi na Chama cha Kudhibiti Silaha kinakadiria kuwa nchi hiyo ina vichwa vya nyuklia 90.

Kila mwaka, Marekani huipa Israel dola bilioni 3.8 kama msaada wa kijeshi chini ya makubaliano ya miaka kumi hadi 2028. 

Askari jeshi wa Israel akiwa katika doriaPicha: Ohad Zwigenberg/AP/dpa/picture alliance

Mnamo Jumapili, waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, alisema ameagiza kupelekwa kwa betri ya mfumo wa ulinzi wa angani THAAD na vikosi vya ziada katika kanda ya Mashariki ya Kati.

Austin ameongeza kuwa ameagiza wanajeshi kadhaa kuwa tayari kuimarisha utayari wao na uwezo wa kutoa majibu ya haraka inavyohitajika endapo kutakuwa na haja kama hiyo.

Soma pia: Borrell aunga mkono kusitishwa mapigano ili kuruhusu misaada kuingia Gaza

Tayari Marekani ilishaipa Israel silaha zaidi na kupeleka meli mbili za kubeba ndege mashariki mwa Bahari Mediterrania.

Lengo la meli hizo mbili, ikiwemo USS Gerald Ford ambayo ndiyo meli kubwa zaidi ya kivita ulimwenguni, pamoja na USS Eisenhower, ni kuzuia mashambulizi ya Hamas na washirika wake Iran na vuguvugu Hizbullah wa Lebanon.

Mnamo Jumanne, Marekani iliwaamuru wanajeshi wake 2,000 kuwa tayari kupelekwa Mashariki ya Kati kama onesho la nguvu.

Uwezo wa kijeshi wa kundi la Hamas

Kundi la Hamas nalo lina zana mbalimbali ambazo limejikusanyia baada miaka mingi.

Vikosi vyake vya kijeshi, vinavyoitwa Brigedi za Ezzedine Al-Qassam, vina wapiganaji 15,000 kulingana na IISS, ingawa inabainisha kuwa vyombo vya habari vya Kiarabu vimeweka idadi hiyo kuwa 40,000.

Wapiganaji wa kundi la HamasPicha: picture alliance / ZUMAPRESS.com

Kundi hilo lina silaha nzito ambazo imepata kutoka washirika wake wa Mashariki ya Kati hususan Iran, Syria na Libya.

Lakini pia limenunua bunduki na zana nyingine kutoka China na nchi nyingine.

Wanamgambo wa Hamas pia wana silaha walizojitengenezea ikiwemo mabomu.

Duru za nchi za Magharibizimesema Hamas pia ina ndege zisizohitaji rubani, mabomu, makombora ya kuelekeza dhidi ya vifaru vya kivita na vifyatua gruneti miongoni mwa zana zake.

Hata hivyo takwimu kamili hazijulikani. Roketi zake nyingi pia zimetengenezwa ndani na ni za kiteknolojia.

Soma pia: Papa Francis ataka vita visitishwe Gaza

Kumekuwa pia na makabiliano ya mpakani kati ya Israel na Lebanon ambako vuguvugu la Hizbullah linaloungwa mkono na Iran lipo.

Mnamo mwaka 2021, kundi la Hizbullah lilidai kuwa na wapiganaji 100,000. Hata hivyo taasisi ya INSS na wachambuzi wa Israel wanasema idadi kamili ni nusu ya takwimu waliyotaja.

Kulingana na Elliot Chapman, mchambuzi wa masuala ya ulinzi kutoka Uingereza, wanamgambo wengi waHizbullah si wapiganaji wa kudumu, bali huitwa tu na kushirikishwa haja inapotokea.

Katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Syria, kundi hilo liliwaita wapiganaji 40,000 na kuwashirikisha.

INSS inasema Hizbullah ina kati ya makombora 150,000 hadi 200,000.
(Chanzo: AFPE)

Israel kuuzingira Ukanda wa Gaza

02:48

This browser does not support the video element.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW