Ugonjwa wa kifafa cha mimba ni miongoni mwa magonjwa hatari unao ondoa maisha ya wanawake wengi waja wazito nchini Tanzania. Ugonjwa huu unashika nafasi ya pili kwa vifo vinavyotokana na uzazi. Dr Living Colman daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ananuchambua ugonjwa huo.