Video ya Kurunzi safari hii inamulika utamaduni wa vazi la kaniki miongoni mwa baadhi ya jamii nchini Tanzania. Je asili ya vazi hili ni wapi? Linavaliwa na kina nani, kwa nini, wapi na thamani yake ni gani? Je ni dhana zipi zilizopo kuhusu vazi hilo na vijana wa leo wanalizungumziaje? Salma Mkalibala na majibu ya hayo pamoja na maelezo zaidi.