Parkinson ni ugonjwa unaoathiri mfumo wa neva katika ubongo, na kusababisha harakati zisizodhibitika kama vile kutetemeka, kukakamaa kwa misuli, na ugumu wa kusawazisha mwili. Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), ugonjwa wa Parkinson umeongezeka mara mbili katika miaka 25 iliyopita, na kufikia zaidi ya milioni 8.5 duniani. #kurunziafya 11.11.2024