1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fainali za AFCON kuchezwa leo mjini Abidjan

11 Februari 2024

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON inakamilika leo Jumapili huku Ivory Coast wakilenga kuandika historia watakapokutana na Super Eagles ya Nigeria kwenye fainali.

Kombe la AFCON
Kombe la AFCONPicha: MOHAMED ABD EL GHANY/REUTERS

Mechi hiyo itaanza saa tatu usiku kwa saa za Ivory Coast kwenye Uwanja wa Olimpiki wa Ebimpe mjini Abidjan, uwanja ambao Nigeria iliwashinda wenyeji hao Ivory Coast 1-0 wakati wa hatua ya makundi.

Baada ya mwezi mmoja, mashindano hayo ya AFCON ambayo yamesisimua zaidi katika kumbukumbu za karibuni, yamewakutanisha vigogo hao wawili wa soka wa Afrika Magharibi.

Miaka 11 baada ya kutangazwa mabingwa wa bara Afrika, Nigeria inalenga kushinda taji lake la nne na kwa kufanya hivyo italingana na wapinzani wa jadi Ghana. Ni Misri pekee iliyoshinda kombe hilo mara saba na Cameroon mara tano ambazo zimeshinda kombe hilo la Afrika mara nyingi zaidi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW